Thursday, January 11, 2018

JK, VIONGOZI MBALIMBALI WAMFARIJI MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU

 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ukiwasili nyumbani tayari kwa ibada maalum ya maombolezo, iliyofanyika jana jioni.
 Huzuni ilitawala pale mwili wa Marehemu ulipowasili Nyumbani.
 Ibada ya kumuombea Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ikiendelea nyumbani.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale Victoria, jijini Dar es salaam jana jioni. Katikati ni Mzee Ally Mtopa.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe wakati walipokutana kwenye Msiba wa Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam jana jioni.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akiwa ameambatana na viongozi Wengine wa Chama hicho waliofika nyumbani wa Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kumfariji kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru.



 Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale Victoria, jijini Dar es salaam jana jioni


















Mheshimiwa Mbowe akisalimiana na Waziri wa zamani wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Nazir Karamagi

No comments: