Friday, April 14, 2017

WAIMBAJI WA TAMASHA LA PASAKA WAANZA KUWASILI LEO,SOLLY MAHLANGU KUWASILI KESHO JIJINI DAR


Pichani kulia ni Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya,Mercy Masika akiimba moja ya wimbo wake ulioitwa Mkono wa Bwana, mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),leo mchana,jijini Dar,Mercy tayari amekwisha wasili jijini Dar tayari kutumbuiza katika tamasha la pasaka litakalofanyika April 16,2017 ndani ya Uwanja wa uhuru,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya Ndani Mh.Mwigulu Nchemba.Pichani shoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama,ambayo ndio waandaaji wa tamasha hilo.
 Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya,Mercy Masika akielezea namna alivyojiandaa kuwakonga mashabiki wake mbalimbali watakaofika katika tamasha la Pasaka hapo Jumapili ndani ya uwanja wa Uhuru,Mercy amesema amejiandaa vyema na amewaomba wapenzi wa Injili wakiwa na familia zao kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo adhimu ikiwemo kumtukuza na Kumuabudu Mungu kwa njia ya Uimbaji.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ,Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo mchana kuelekea kwenye kilele cha tamasha la Pasaka,linalotarajiwa kufanyika jumapili hii April 16,2017,katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.Msama amesema kuwa kila kitu kimekamilika na Waimbaji watakaotumbuiza katika tamasha hilo wanaendelea kujiandaa vilivyo,na walioko nje ya nchi tayari wameanza kuwasili akiwemo Muimbaji Mercy Masika kutoka nchini Kenya,na kesho wanawasili waimbaji wengine akiwemo muimbaji nyota kutoka Afrika Kusini Solly Mahlangu na skwadi lake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ,Alex Msama,Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya,Mercy Masika na Mdau wa nyimbo za injili wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na wana habari,mapema leo mchana jijini Dar.

No comments: