Wednesday, April 12, 2017

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUZINDUA KLABU ZA ELIMU YA UZIMAJI MOTO SHULE ZA SEKONDARI NCHINI


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Thobias Andengenye, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali(hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kueleza mipango mbalimbali ya jeshi hilo ikiwemo uzinduzi wa klabu katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo),jijini Dar es Salaam leo, Kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi, Casmir Ndambalilo. 

Mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wakuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikiwemo uzinduzi wa klabu katika shule za sekondari, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, akiuliza swali kwa Kamishna Jenerali wa jeshi hilo,Thobias Andengenye(hayupo pichani), wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo. 
Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wakuelezea mipango mbalimbali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikiwemo uzinduzi wa klabu katika shule za sekondari nchini, zitakazotoa elimu ya uzimaji moto kwa wanafunzi, wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye wakati wa mkutano huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari(Maelezo), jijini Dar es Salaam leo. 

Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments: