Tuesday, April 18, 2017

DAWASCO WATAKIWA KUONGEZA KASI YA USAMBAZAJI WA HUDUMA YA MAJI DAR


fisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo wakati alipotembelea kampuni hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
A 1
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akimtembeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo katika baadhi ya ofisi za kampuni hiyo wakati alipotembelea kampuni hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
A 2
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto)akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo wakati alipotembelea kampuni hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
A 3
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akieleza kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo, mipango na mikakati ya kampuni hiyo katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama katika jiji la Dar es Salaam wakati Katibu Mkuu alipotembelea kampuni hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
A 5
Baadhi ya watumishi wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO)pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) wakifuatilia kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo wakati alipowatembelea mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
A 6
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Archad Mutalemwa (kulia) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) wakati Katibu Mkuu alipokutana na watedaji wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA), katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja.
A 8
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akizungumza na watendaji wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) wakati alipowatembelea mapema hii leo katika Ofisi za DAWASCO jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
…………..
Na: Frank Shija – MAELEZO.

Kampuni ya Usambazaji wa Maji Dar es Salaam (DAWASCO) pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) zatakiwa kuongeza kasi ya usambazaji kwa wananchi ili kufikia malengo ya Serikali katika kuwatumikia wananchi wake kwa kuwapa huduma za msingi.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo wakati akiongea na Menejimenti ya Mamlaka hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Profesa Kitila amesema kuwa licha ya ongezeko la upatikanaji wa maji, ipo vhangamoto ya idadi kubwa ya wananchi kutofikiwa na huduma hivyo hivyo ni lazima sasa Mamlaka husika kuongeza kasi ya usambazaji wa miundombinu ya maji katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa.

“Pamoja na kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha upatikanaji wa maji hakikisheni mnaongeza kasi ya usambazaji wa huduma hii muhimu kwa wananchi, kwakufanya hivyo mtakuwa mnatendea haki dhana ya kuwa mnaongoza kwa mapato lakini pia mnatoa huduma stahiki kwa wananchi,” alisema Profesa Kitila.

Aidha Profesa Kitila ametoa rai kwa wateja wote wa Dawasco na Dawasa zikiwemo taasisi za umma kutii agizo la Mhe. Rais kwa kulipia huduma wanazopatiwa ili kuziwesha mamlaka hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji wa Maji Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa katika kuhakikisha uzalishaji wa maji umeongezeka kwa kutoka lita za ujazo wa mita 160 Milioni kwa siku hadi kufikia lita za ujazo mita 271Milioni kwa siku ambazo ni sawa na asilimia 100.37% ya lengo la upatikanaji wa maji ambalo ni lita 270 Milioni kwa siku.

Mhandisi Luhemeja aliongeza kuwa jumla ya Vizimba 560 (Gati za kuuzia maji) vimeunganishwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi ikiwa ni muendelezo wa kuongeza kasi ya usambazaji na upatikanaji wa huduma ya maji miongoni mwa jamii.

Katika hatua nyingine Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema kuwa katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kuhakikisha wanakina mama wanatua ndoo za maji kichwani Dawasco inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi wa kuongeza usambazaji wa huduma ya maji katika eneo la takribani 1,427Km unaohusisha maeneo ya Tegeta, Mpiji hadi Bagamoyo ifikapo mwezi Julai mwaka huu ambapo tayari fedha Tsh. 117Bilioni kwa ajili ya mradi huo zimepatikana kupitia Benki ya Dunia.Mradi huo utakapokamilika unakadiriwa kuongeza idadi ya watumiaji wa maji takribani laki moja.

Katika kuhakikisha inafikia azma ya kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma ya maji kwa wananchi Dawasco inaendesha Kampeni ijulikanayo “Mama Tua Ndoo ya Maji Kichwani Ndani ya Siku 90” ikiwa na lengo la kuwaunganisha na huduma ya maji wateja takribani 151,000 wataunganishwa na huduma hiyo katika eneo linalopakana na Barabara ya Morogoro. Kampeni hiyo imeanza kuanzia tarehe 1 Aprili hadi 30 Juni, 2017.

No comments: