Sunday, March 12, 2017

WANANCHI WA MKURANGA WAPATA HUDUMA ZA VIPIMO VYA AFYA ZAO BURE

Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan  Tanzania, Othman Kaporo akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) wakati wa upimaji wa afya kwa wananchi wa Wilaya ya Mkuranga leo.
  Muuguzi Mariam Adamu akipima kipimo cha Sukari na Msukumo wa Damu
 Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii 

Wananchi wa Mkuranga wametakiwa kujitokeza kupima magonjwa mbalimbali na pale wanapokutwa kuweza kutibu kwa wakati mwafaka.

Akizungumza katika upimaji wa Afya huo,Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan  Tanzania, Othman Kaporo amesema kuwa katika dunia ya sasa jamii inawajibu wa kupima afya kujua ana tatizo au hana ili kuweza kuchukua hatua pamoja na kujinga na magonjwa mbalimbali yanatokana na mfumo wa maisha.

Othman amesema kuwa huduma hiyo itatolewa  kwa wa wananchi wa Mkuranga, Vikindu, Mwanambaya, Mbagala na maeneo  mengine yaliyo karibu.

Amesema wamechagua Wilaya hiyo kutokana watu wengi wanashindwa kuifikia na kuona kwa taasisi hiyo inawajibu wa kupima afya za wananchi ha.

Aidha amesema kuwa watu wengine ambao wanauwezo wajitokeze katika kutoa huduma ya upimaji ili waweze kujikinga na magonjwa ambayo yanatokana na mfumo wa maisha.

Amesema tangu jana walipoanza kupima watu zaidi ya 500 wamwjitokeza kupima na mwitikio umekuwa  mkubwa wa kuweza kuvuka malengo ya upimaji huo.

Huduma ya vipimo walivyotoa ni Msukumo wa Damu (BP), Sukari , Unene na Urefu kuendana sawa na mwili (BMI) Ushauri Nasaha  na Upimaji wa VVU,Utafiti wa Saratani ya matiti pamoja na utafiti wa Saratani ya Kizazi.
 Wananchi wakisubiri huduma ya vipimo vinavyotolewa na Taasisi ya Ibun Jazar leo.

No comments: