Tuesday, March 21, 2017

Airtel yazindua HATUPIMI bando, Ongea bila kikomo


 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Wa (pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako
 Wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia) ,  Niki wa Pili (katikati) na Gnako wakitumbuiza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ya Airtel ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja Airtel kuongea bila kikomo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akisisitiza jambo  wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo
 Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (wa pili kushoto)  na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako kwa pamoja  wakizindua Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua OFA kabambe ijulikanayo kama HATUPIMI Bando itakayowawezesha wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.
“Airtel HATUPIMI Bando” itapatikana katika vifurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi vilivyosheheni dakika zisiso na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi kwa kuwa hakuna kupimiwa dakika za maongezi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii kabambe, Mkurugenzi wa Masoko, Isack Nchunda alisema “ Airtel Hatupimi, sasa Hatupimi dakika zenu za maongezi, tunaleta huduma hizi nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa kuwapatia thamani ya pesa zao katika huduma na bidhaa zetu.

“HATUPIMI Bando” itawapatia wateja wetu nchi nzima uhuru wa kuongea na familia, marafiki na wadau wa biashara zao kulingana na aina ya kifurushi mteja alichochagua ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi bila kujali vifurushi vyao kuisha muda wa maongezi. Kuna vifurushi vya Hatupimi kwa siku vya hadi shilingi 1000/= pia vipo vya wiki kwa shilingi 5000, na vilevile unaweza kujiunga na HATUPIMI kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= ili ufurahie huduma yakutopimiwa dakika zako ongea bila kikomo

Airtel tunaamini “HATUPIMI” ni ofa ya kipekee sokoni, tunatoa wito kwa wateja wetu na wateja wapya kujiunga sasa na kufurahia ofa hii kabambe inayowapa uhuru wakuonge watakavyo bila kikomo. Aliongeza Nchunda

Kujiunga na ofa ya HATUPIMI Bando piga *149*99# kisha chagua 1 kupata HATUPIMI kisha chagua bando ya Siku, Wiki, Mwezi kulingana na mahitaji yako “ alisisitiza Nchunda.

Airtel imekuja na ofa yake ya HATUPIMI ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzindua ofa kabambe kupitia huduma ya Airtel Money, Vile vile airtel wiki hii ilizindua kampeni ya kufungua maduka yake 2,000 yatakayotoa huduma kwa wateja ili kuwafikishia wateja wake wote huduma zao popote walipo.

No comments: