Tuesday, February 14, 2017

WANAHABARI TUMUUNGE MKONO RAIS KATIKA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA.

KUNI
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau Redio na vyombo vya habari kwa ujumla katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amevishauri vyombo vya habari nchini kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo Kikuu huria cha Tanzania na kusisitiza kuwa vyombo vya habari viwe sehemu ya kuwaunganisha watanzania katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
“Wanahabari tuliunganishe taifa letu tuwe kitu kimoja katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya” alisisitiza Mhe. Nnauye.
Ameongeza kuwa sasa ni wakati wa watu wote kuungana kwa pamoja zikiwemo tasnia zilizopo katika Wizara yake za Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwani vita hii ni ya watanzania wote na sio mtu mmoja au Serikali pekee.
Aidha Mhe. Nape amevitaka vyombo vya habari kutobaki nyuma katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na kuhakikisha  haki inatendeka na vita dhodi ya madawa ya kulevya vinashinda.

No comments: