Tuesday, February 14, 2017

NAPE: WANAHABARI SOMENI NA KUZIELEWA SHERIA ZINAZOHUSU TASNIA YA HABARI.

NAPE2
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau Redio na vyombo vya habari kwa ujumla katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
NAPE3
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa Dkt. Ayub Riyoba akitoa hoja kuhusu umuhimu wa Redio katika kuunganisha jamii ya watanzania katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
NAPE4
Mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Bibi Zulmira Rodrigues akitoa neno la kwa Serikali na wadau wa Redio na vyombo vya habari nchini katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
NAPE5
Mkurugenzi wa Utangazaji Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Fredirick Ntobi akifafanua jambo kwa wadau wa Redio Redio kuhusu Redio za jamii katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
NAPE6
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na Mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Bibi Zulmira Rodrigues wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
NAPE7
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Bibi Zulmira Rodrigues  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
NAPE8NAPE9
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea risala kutoka kwa Mwakilishi wa Redio za Jamii nchini Bw. Baraka David wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
NAPE10
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Bibi Zulmira Rodrigues  na wawakilishi wa vyombo vya habari nchini hususani Redio mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya Siku ya Radio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
……………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewashauri waandishi wa habari nchini kuwa na utaratibu na desturi ya kusoma na kuelewa Sheria mbalimbali zinazoendesha tasnia ya Habari nchini.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo Kikuu huria cha Tanzania na kusisitiza kuwa usomaji wa Taratibu na Sheria utasaidia kuondoa mikanganyiko inayojitokeza mara kwa mara kuhusu mambo mbalimbali.
“Nadhani wanahabari wanapaswa kuwa na maswali mengi katika jambo unaloambiwa husiamini kila kitu unachoambiwa pata muda wa kusoma na kujiridhisha”Alisistiza Mhe. Nnauye.
Ameongeza kuwa kila mwanahabari nchini ana jukumu la kuzisoma kwa kina na kuzielewa Taratibu na Sheria zinazoendesha tasnia ya habari nchini na kama kuna Sheria yoyote ina mapungufu basi yawasilishwe kwake na kujadiliwa ili yafanyiwe marekebisho.
Aidha Mkurugenzi wa Utangazaji Kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Fredirick Ntobi awaomba wadau wa habari nchini kuendelea kutoa ushirikiano kwao katika kuendeleza jitihada za kuifanya sekta ya habari nchini kuendelea kuwa mubimu katika maendeleo ya taifa.
“Niwaombe wadau wa habari nchini tuendelee kushirikiana kwa dhati katika hili tusome Taratibu na Sheria zilizopo na kuendelea kutoa maoni yetu pale ambapo kuna mapungufu ili tuboreshe na kuiendelezaTasnia  hii ya habari” Alisisitiza Bw. Ntobi.

No comments: