Thursday, December 01, 2016

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NA MKURUGENZI TBA WAKAGUA MAENEO YATAKAYOJENGWA NYUMBA ZA ASKARI WA JESHI LA MAGEREZA JIJINI DAR

kami1
Kamishna Jenerali wa Magereza – CGP. John Casmir Minja(katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo, Bw. Elius Mwakalinga wakiangalia moja ya eneo la Gereza Segerea ambalo litajengwa nyumba za kuishi za Maafisa na askari wa Jeshi hilo(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Kuu Segerea, ACP.  Godfrey Kavishe akiwaonesha eneo hilo walipofanya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali ya Jeshi ambapo tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa Bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika Mkoa wa Dar es Salaam.
kami2
Moja ya eneo litakalojengwa nyumba za Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza lililopo katika eneo la Gereza Kuu Segerea, Jijini Dar es Salaam kama linavyoonekana katika picha.
kami3
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo, Bw. Elius Mwakalinga akisalimiana na Baadhi ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Dar es Salaam alipofanya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali yatakayojengwa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo leo Novemba 30, 2016. 
kami4
Kamishna Jenerali wa Magereza – CGP. John Casmir Minja(wa pili kulia) akiwa ameongozana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu pamoja na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo waliopo katika Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kuanza kutembelea maeneo mbalimbali yatakayojengwa nyumba za watumishi wa Jeshi hilo. 
kami5
Moja ya nyumba ya mabati iliyopo katika Gereza la Mahabusu Keko kama inavyoonekana katika picha. Katika kukabiliana na uhaba wa nyumba za askari wa Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa Bilioni 10 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika Mkoa wa Dar es Salaam.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments: