Monday, October 03, 2016

NHC YAKABIDHI MADARASA SHULE YA MSINGI SAKU WILAYA YA TEMEKE

1Meya wa Halmashauri ya Temeke Abdallah Chaurembo akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa madarasa ya shule ya msingi Chamazi Saku wilayani Temeke wakati wa makabidhiano yaliyofanyika shuleni hapo, Madarasa hayo yamejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC kwa gharama ya shilingi milioni 32 , makabidhiano hayo yamefanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Nassib Mmbaga, Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Shirika la Nyumba na Huduma kwa Jamii wa NHC Susan Omari na Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Felix Lyaviva2Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba NHC Susan Omari akifungua mlango mara baada ya makabidhiano hayo kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw. Nassib Mmbaga na kushoto ni Meya wa Halmashauri ya Temeke Abdallah Chaurembo.3Haya ndiyo madarasa yaliyojengwa na Shirika la Nyumba NHC kwa gharama ya shilingi Milioni 32 katika shule ya msingi Chamazi Saku.5Baadhi ya wanafunzi wakikokotoa hesabu walizopewa na Mh. Meya wa Manispaa ya TemekeHalmashauri ya wilaya ya Mh. Temeke Abdallah Chaurembo.6Mheshimiwa Meya wa Manispaa ya Temeke Halmashauri ya wilaya ya Mh. Temeke Abdallah Chaurembo akifundisha hesabu darasani kukumbushia hesabu alizokuwa amebobea enzi hizo.7Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Shirika la Nyumba NHC Susan Omari akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake mara baada ya makabidhiano ya madarasa hayo.8Mh. Meya wa Manispaa ya Temeke Halmashauri ya wilaya yaMheshimiwa Temeke Abdallah Chaurembo akikabidhi vitabu kwa mwanafunzi Leokadia Projestus wa darasa la sita shule ya msingi Chamazi Saku katikati ni Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Shirika la Nyumba NHC Susan Omari.9Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Felix Lyaviva akizungumza na wanafunzi.1011Mwanafunzi Leokadia Projestus wa darasa la sita shule ya msingi Chamazi Saku akitoa hotuba kwa niaba ya wanafunzi wenzake.

No comments: