Wednesday, October 12, 2016

MAELFU WASHIRIKI KATIKA MATEMBEZI YA AMANI YA SIKU YA ASHURA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Sheikh  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim (wa tatu kutoka kushoto) akiongoza matembezi ya Amani ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae ni Imam Hussen (a.s) leo jijini Dar es Salaam. Siku ya mwezi 10 Muharram inajulikana kama ni siku ya Ashura. Imamu Husain (a.s.) aliuliwa kikatili pamoja na wafuasi wake wachache na ndugu zake. Masaibu haya yalitokea zaidi ya miaka 1300 iliyopita huko Kerbala (karibu na mji wa Baghdad katika nchi iitwayo Iraq hivi sasa). 
 Sehemu ya maelfu ya Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika matembezi ya Amani ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)  Imam Hussen(a.s) leo jijini Dar es Salaam.
 Matembezi yakiendelea leo jijini Dar es Salaam.
 Mzungumzaji na Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania,Sheikh Hemed Jalala akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  matembezi ya Amani ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Imam Hussen(a.s) leo jijini Dar es Salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim akizungumza wakati wa  matembezi ya Amani ya kuadhimisha kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Imam Hussen(a.s) leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

No comments: