Friday, August 05, 2016

WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA BANDA LA NHC MAONESHO YA WAKULIMA (NANE NANE) KITAIFA MKOANI LINDI

Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi, Mussa Patrick Kamendu akitoa maelezo ya namna miradi ya NHC inavyoendeshwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), George Simbachawene akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego wanaofuatilia maelezo kutoka kwa meneja huyo wakati wa maonesho ya NaneNane yanayoendelea viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. NHC imeshiriki maonesho hayo ya NaneNane yaliyofunguliwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo yakiwa na kauli mbiu “Kilimo, mifugo na uvuvi ni nguzo ya maendeleo. 
Waziri George Simbachawene akiweka saini katika kitabu cha wageni katika banda la NHC wakati alipotembelea banda hilo hapo jana pembeni yake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akifuatilia tukio hilo.
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Lindi, Mussa Kamendu akimkaribisha Mheshimiwa Waziri George Simbachawene katika maonesho ya Nanenane eneo la Ngongo. NHC imeshiriki maonesho hayo ya NaneNane yaliyofunguliwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo yakiwa na kauli mbiu “Kilimo, mifugo na uvuvi ni nguzo ya maendeleo. 
Waziri Simbachawene alipotembelea banda la NHC wakati wa maonesho ya NaneNane yanayofanyika eneo la Ngongo mkoani Lindi hapo jana.
Waziri, George Simbachawene akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi,  Godfrey Zambi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Lindi, Mussa Patrick Kamendu wakati wa maonesho ya NaneNane yanayoendelea mkoani Lindi.

No comments: