Thursday, August 04, 2016

TAUSI LIKOKOLA KUZINDUA KIPINDI CHAKE ‘TAUSI LIKOKOLA’S AFRICAN PRINCESS MODEL SEARCH’

Mwanamitindo mstaafu wa kimataifa Tausi Likokola, ambaye yupo hapa nchini,akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi kipindi chake cha Television, chenye malengo ya kuwainua wasichana na wanamitindo kwa jumla kwa kutumia ulimbwende, fasheni na uanamitindo kama mwamvuli kitakachojulikana kwa jina la ‘TAUSI LIKOKOLA’S AFRICAN PRINCESS MODEL SEARCH’. PICHA NA MICHUZI JR.

Tausi ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kukuza vipawa vya wasichana ulimwenguni kote kwa kutumia uzoefu wake katika fasheni, mitindo uandishi wa vitabu na ujasiriamali, anasema ni wakati sasa wa kufanya hayo hapa nyumbani kwao mwenyewe. Amesema kuwa kipindi hicho kimetokana na wazo lililobebwa katika vitabu vyake viwili, T’he African Princess’ na kingine cha ‘Beautiful You’."Lakini pia kipindi hicho cha kwanza na cha aina yake, kitaanza kurushwa katika kituo cha televisheni cha TV1 kuanzia Ijumaa ya Agosti 5, 2016 saa 10:00 jioni na kurejewa tena Jumapili asubuhi"amesema Likokola.

Tausi anasema kuwa wasichana wanahitaji kufundishwa na kutiwa moyo kuelekea katika ndoto zao,hivyo kipindi hicho kitaonesha vipengele tofauti tofauti katika maisha kuanzia maadili, ulimbwende, nidhamu na mambo mengine, hiki ni kipindi kwa familia nzima,huku akibainisha lengo kuu la Tausi Likokola’s African Princess Model Search ni kukuza na kuongeza uwezo wa msichana mmoja mmoja katika stadi za uongozi na uwezo katika kujitambua, kujikubali, kujiamini na kuwa na mawazo chanya na kujifunza stadi za mawasiliano mazuri ambayo hatimaye yatafanya washindani kufanikiwa sana katika maisha yao ya baadaye katika ulimwengu wa ushindani wa fasheni.
Tausi aliyezindua bidhaa kadhaa za urembo na maisha kupitia kampuni yake iliopo Tanzania,ijulikanayo kama ‘Tausi Dreams Ltd ambaye bado anayeishi Marekani,akionesha nywele zake ikiwa ni moja ya bidhaa ilioko kwenye miradi yake mbalimbali ikiwepo pafyumu yake inayoitwa Tausi Dreams,nywele za binadamu zinazoitwa Tausi Beautiful You Hair.Pichani kushoto ni Muwakilishi wa Tausi hapa nchin,Bi. Margaret Bitungwa na kulia ni Mmoja wa Wakilishi wa Tv1 kutoka kitengo cha Masoko,Edgar Wilson.
Mmoja wa Wakilishi wa Tv1 kutoka kitengo cha Masoko,Edgar Wilson akifafanua zaidi kuhusiana na muda na mambo mbalimbali yatakayokuwa yakirushwa hewani kupitia kipindi hicho kitakachojulikana kwa jina la ‘TAUSI LIKOKOLA’S AFRICAN PRINCESS MODEL SEARCH’
Tausi Likokola akionesha moja ya kitabu kati ya viwili ambavyo aliviandika The African Princess’ na kingine cha ‘Beautiful You’.

Tausi aliyekulia katika ulimwengu wa fasheni kimataifa katika miaka ya 90, amefanya kazi na makampuni makubwa ya mitindo kama Gucci, Christian Dior, Issey Miyake, Tommy Hillfger, Escada na wengine wengi, na sura na kazi zake kupamba kurasa za mbele na za ndani katika magazeti na majarida kadhaa ya mitindo na maisha ya kimataifa na hapa nyumbani, amekuwa akiwatia moyo wanamitindo wengi hapa nchini na wengine duniani kote.

Tausi amefanikiwa sana kulitumia jina na kipawa chake kuwasaidia watu wake wa Tanzania katika elimu, kutambua UKIMWI, mahitaji ya jamii, na ameweza kuchangia katika kukua kwa utalii katika nchi yake ya kuzaliwa (Tanzania), kibiashara na kukuza maliasili. Tausi ana mpango wa kusimamia kazi kadhaa za kujitolea kupitia kampuni yake ya ‘Tausi and Friends for Life’

Tausi alipumzika kujitokeza katika uanamitindo ili kupata muda mzuri wa kukaa na familia. Wakati wa kazi za mitindo Tausi ametembelea nchini nyingi za Afrika, Ulaya, Asia, Australia na kwa sasa akiwa anaishi Marekani. Tausi ameandika vitabu vinne hadi sasa akitumia uzoefu wake uliopata toka mataifa mbalimbali akifanya kazi na wasichana toka ulimwenguni kote kuwasaidia kwa hali na mali. Vitabu alivyotoa hadi sasa ni; The Art of the Beauty and Health’, The African Princess,’ ‘The Touch of an Angel’ na ‘Beautiful You’.

No comments: