Friday, August 19, 2016

RC MRISHO GAMBO ADHAMIRIA KUKOMESHA VITENDO VYA UCHOMAJI MOTO MASHULE


Mkuu wa Mkoa Mteule wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Mrisho Gambo anaziba nafasi ya Mhe. Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Agosti.
Mkuu wa Mkoa Mteule wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akisaini kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Mrisho Gambo anaziba nafasi ya Mhe. Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Agosti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo wakati akimuapisha Mkuu wa Mkoa Mteule wa Arusha Bw. Mrisho Gambo Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Mrisho Gambo anaziba nafasi ya Mhe. Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Agosti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Mkuu wa Mkoa Mteule wa Arusha Bw. Mrisho Gambo wakati akimuapisha Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Mrisho Gambo anaziba nafasi ya Mhe. Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Agosti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za kumuapisha Mkuu wa Mkoa Mteule wa Arusha Bw. Mrisho Gambo Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Mrisho Gambo anaziba nafasi ya Mhe. Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Agosti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mh. Suleiman Jafo wakati wa sherehe za kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Mrisho Gambo anaziba nafasi ya Mhe. Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Agosti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Mrisho Gambo anaziba nafasi ya Mhe. Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Agosti.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo (Kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, wakati wa sherehe za kula kiapo Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Mrisho Gambo anaziba nafasi ya Mhe. Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Agosti katikati ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baadaya kula kiapo Ikulu jijini Dar es salaam. Bw. Mrisho Gambo anaziba nafasi ya Mhe. Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Agosti.PICHA NA HASSAN SILAYO


Na Jonas Kamaleki

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amedhamiria kukomesha vitendo vya uchomaji moto mashule mkoani humo ili kuondoa hofu kwa wanafunzi na kuwawekea mazingira mazuri ya kusomea. 

Akizungumza baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Gambo amesema kuwa atafanya kila liwezekanalo kuwasaka na kuwakamata wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha mahakamani ili wachukuliwe hatua za kisheria. “Tumechoka na hali hii ya kila kukukicha kusikia matukio ya shule kuungua moto kwa hiyo tutaweka ulinzi wa uhakika katika shule za bweni na hosteli ili kuzuia vitendo viovu”, alisema Gambo. 

Gambo amesema kuwa akiwa Mkuu wa Mkoa atahakikisha anasimamia utekelezaji wa vipaumbele vya Taifa kama Elimu bure, ajira kwa vijana, kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha maisha ya wananchi hasa wa hali ya chini. 

Gambo Mrisho ameapishwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha baada ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Felix Ntibenda Kijiko uteuzi wake kutenguliwa. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo amesema kuwa Wizara yake kwa sasa inafanya kazi ya kuondoa watumishi hewa na kupinga vikali ufanyaji kazi kimazoea. 

“Lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi na kuondoa ubinafsi tuliourithi”, alisema Jafo. 

Aidha, Jafo amesema wapo watu waliokuwa wanahakikisha wanafanya kila liwezekano kutumia ofisi zao kujinufaisha, na kuongeza kuwa watu hao inabidi wajiondoe haraka au wataondolewa. Kuhusu walioongeza majina ya wanafunzi hewa ili kujipatia vipato, Jafo amesema anawatafuta na wakibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

No comments: