Monday, October 15, 2012

MWILI WA KAMANDA LIBERATUS BARLOW WAAGWA LEO NYAMAGANA JIJINI MWANZA


            Mabanda ambayo watu wamekaa kwa utulivu wakiuaga mwili wa Kamanda Liberatus Barlow.
Umati mkubwa watu wakiwa katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Liberatus Barlow.
Afande George Msangi akiongoza ratiba za kumuaga aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Liberatus Barlow aliyeuawa usiku wa kuamkia Jumamosi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri karibu na hoteli ya Tai Five.
 Msafara wa magari ya kuleta mwili wa marehemu Liberatus Barlow yakiingia katika uwanja wa Nyamagana ili viongozi na wananchi mbalimbali wapate kuuaga mwili huo.
                               Magari yakiingia katika uwanja wa Nyamagana.
 Maaskari walioteuliwa kubeba mwili wa marehemu Liberatus Barlow wakiwa wamejipanga vyema ili mwili uweze kutolewa ndani ya gari ili uwekwe sehemu nzuri ambayo kila mtu anaweza kuuaga vizuri.
                      Hapa wakiushusha kutoka ndani ya gari ili waweze kuubeba.
            Safari ya kuelekea sehemu maalum iliyopangwa kwa ajili ya mwili wa marehemu ilianza hivi.
                          Maaskari wakiwa sawa kutekeleza jukumu lao.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Everest Ndikillo akielekea kuuaga mwili wa marehemu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow katika uwanja wa Nyamagana leo.
 Viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakisimama kwa dakika chache kuupa heshima mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow.
             Baadhi ya Maafisa ya Jeshi la Polisi.
                Ofisa Usalama wa Taifa, Meja Jacob Mutashi mwenye suti nyeusi kulia akionekana pichani.
                     Mwili wa Marehemu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.
 Mwandishi Peter Fabian kutoka gazeti la Mtanzania akiweka vizuri picha ya marehemu Kamanda Liberatus Barlow.
 Saluti kutoka kwa Maofisa wa Polisi kwa Marehemu Kamanda wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga akiweka saini katika daftari la maombolezo katika msiba wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow katika uwanja wa Nyamagana.
 Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Richard Manumba akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Bi. Jackline Wana huku Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bi. Rosemary Mwanyika akiwa mbele mwenye suti nyeusi.
 Ibada ya kuuaga mwili Marehemu, Kamanda Liberatus Barlow kama ilivyoongoza na Watumishi wa Kanisa la Roman Catholic maana kamanda alikuwa muumini wa kanisa hilo.
 Wakuu wa wilaya mbalimbali katika Mkoa wa Mwanza na baadhi ya viongozi wa serikali, vyama vya kisiasa wakionekana katika picha wakiwa na majonzi mazito.
 Wananchi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Mwanza na nje ya Mkoa wa Mwanza wakionekana katika tukio la kuuaga mwili wa Kamanda Liberatus Barlow.
 Wanafamilia wa marehemu, Kamanda Liberatus Barlow wakiwa na majonzi makubwa sana katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao.
 Maafisa wa Majeshi aina mbalimbali kutoka Tanzania wakionekana katika hafla la kuuaga mwili wa marehemu, Kamanda Liberatus Barlow.
            Mabanda ambayo watu wamekaa kwa utulivu wakiuaga mwili wa Kamanda Liberatus Barlow.
Umati mkubwa watu wakiwa katika uwanja wa Nyamagana wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Liberatus Barlow.
(Picha zote kwa hisani ya B Plus Blog)

No comments: