Friday, April 30, 2010

Kapuya arusha kete zake


Serikali.......Viwango vya mshahara kima cha chini sekta binafsi vyatangazwa
WAKATI zikiwa zimebakia siku nne kabla ya kuanza kwa mgomo wa wafanyakazi wote ulioitishwa na Tucta, serikali jana ilitangaza viwango vipya vya kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi, lakini hali inaonekana kuwa ngumu kwa wafanyakazi wa serikalini.
Awali Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Prof Juma Kapuya alitangaza kuwa serikali ingetoa tamko kuhusu kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wa serikalini kabla ya Mei mosi, lakini hakuweza kufanya hivyo jana na badala yake aliibuka na mishahara ya sekta binafsi.
Lakini, jana Kapuya alisema walikuwa wakiendelea na mazungumzo kati ya serikali na wawakilishi kutoka vyama vya wafanyakazi kwenye kikao cha utatu kilichoitishwa na Baraza la Upatanishi (Lesco), ili kujadili hoja hizo saba zilizotangazwa na Tucta.
Waziri Kapuya aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tamko namba 233 la serikali la kima cha chini cha mshahara lililotolewa mwaka 2007 limefutwa na kuanzia leo linatumika tamko jipya namba 172 la kima cha chini cha mshahara la mwaka 2010.
Alisema viwango hivyo vya mishahara ya wafanyakazi wa sekta binafsi, linawagusa wafanyakazi wote katika sekta hiyo.
Profesa Kapuya alisema kuwa katika sekta ya kilimo kima cha chini cha mshahara ni Sh70,000 ikiwa ni ongezeko kutoka Sh50,000, wakati sekta ya biashara na viwanda kima cha chini ni Sh80,000, kima cha chini kwa sekta ya mawasiliano na usafirishaji wa huduma za anga mshahara ni Sh350,000 na wasafirishaji wa mizigo (clearing and forwarding) ni Sh230,000.
Kwa mujibu wa tamko hilo, kima cha chini kwa sekta ya mawasiliano ya simu ni Sh300,000, wakati kima kipya cha chini kwa sekta ya usafiri wa nchi kavu (makondakta na madereva) Sh150,000 na meli za uvuvi ni Sh165,000.
Wafanyakazi wa majumbani wamegawanywa katika makundi matatu ambayo ni wanaofanya kazi kwa mabalozi kima cha chini ni Sh90,000; wanaowafanyia maofisa wanaolipiwa huduma hiyo na waajiri wao ni Sh 80,000 na wengine Sh65,000.
Kima cha chini kwa wanaofanya kazi za hoteli za kitalii ni Sh150,000 na hoteli za kati Sh100,000 wakati hoteli ndogondogo, baa, nyumba za wageni na migahawa ni Sh80,000.
Katika sekta ya madini, upande wa migodi mikubwa, wafanyakazi watalipwa Sh350,000, wachimbaji wadogo, ambao walikuwa wakilipwa Sh80,000, sasa watalipwa Sh150,000, wakati kima cha chini kwa sekta ya biashara na usafirishaji madini ni Sh250,000, huku madalali katika sekta ya madini wakilipwa Sh150,000.
Katika sekta ya biashara na viwanda, kima cha chini ni Sh80,000, sekta ya ulinzi binafsi, kampuni za kigeni ni Sh105,000 na kampuni nyingine Sh80,000, huku kima cha chini kwenye huduma ya afya kikipangwa kuwa Sh80,000
Alisema katika sekta ambazo hazikutajwa, kima cha chini kitakuwa Sh80,000.
Profesa Kapuya alisema mwajiri haruhusiwi kulipa chini ya viwango vilivyotajwa, lakini anaweza kukiongeza kwa kadri anavyopenda ili kuboresha hali za wafanyakazi wao.
“Waajiri wajitahidi kutekeleza kama vilivyotangazwa na serikali ili kuepusha migogoro mbalimbali sehemu za kazi,” alisema Profesa Kapuya.
Kuhusu mgomo wa wafanyakazi wote uliopangwa kuanza Mei 5, Kapuya alisema serikali ilikuwa inaendelea na mazungumzo na Tucta juu ya kima cha chini cha wafanyakazi wa serikalini. Awali, Kapuya aliahidi kutoa tamko hilo kabla ya Mei mosi. Habari imendikwa na Felix Mwagara. SOURCE

Matangazo ya kidato cha sita yatangazwa



SHULE za sekondari za serikali zimeng'ara katika matokeo ya kidato cha sita baada ya wanafunzi wake tisa kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora kitaifa.
Lakini shule hizo za serikali hazikuweza kufua dafu kwa upande wa wasichana baada ya shule binafsi kutoa wanafunzi nane kati ya kumi bora waliofanya vizuri kwenye mtihani huo wa kumaliza elimu ya juu ya sekondari.
Wanafunzi wote walioshika nafasi kumi za kwanza ni wavulana. Wanafunzi hao ni Japhet John wa Shule ya Sekondari ya Ilboru, Manyanda Chitimbo (Kibaha, Pwani), Hassan Rajab (Minaki, Pwani), Abdulah Taher, Stinin Elias, Paul Nolasco na Ephraim Swilla wote kutoka Mzumbe, Morogoro.
Wengine ni Alexander Marwa na Benedicto Nyato kutoka Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Tabora, wakati Samuel Killewo wa Shule ya Sekondari ya Feza Boys ndiye mwanafunzi pekee kutoka shule binafsi aliyeingia kumi bora.
Kwa upande wa shule za wasichana, Jacqueline Seni wa Shule ya Sekondari ya Marian Girls iliyo Bagamoyo mkoani Pwani ndiye aliyeongoza akiwa na wenzake Khadija Mahanga, Esther Mlingwa, Perpetua Lawi na Lilian Kakoko, wakati Gerida John na Subira Omary wanatoka Shule ya Sekondari Dakawa.
Wasichana wengine waliofanya vizuri ni Elaine Kinoti kutoka Ashira, Kilimanjaro, Ruth Pendaeli kutoka Shule ya Sekondari ya Morogoro na Cecilia Ngaiza kutoka St Joseph Ngarenaro, Arusha Cecilia.
Shule za Marian Girls, Mzumbe, Kibaha, Tabora Boys, Ilboru, Malangali, Kifungilo, Tukuyu, Feza Boys na Uru Seminary zimeingia katika kumi bora wakati shule ya High-View International, Fidel Castro, Sunni Madressa, Neema Trust, Mtwara Technical, Muheza, Tarakea, Uweleni, Arusha Mordern na Maswa Girls zimekuwa shule kumi zilizoshika mkia.
Jumla ya watahiniwa 55,764, ambao ni asilimia 88.86 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo mwaka huu, wamefaulu na kati ya hao wasichana waliofaulu ni 21,821 (sawa na asilimia 90.39) ya waliofanya mtihani na wavulana waliofaulu ni 33,943 (sawa na asilimia 87.90 ya wavulana waliofanya mtihani).
Kwa kulinganisha na mwaka jana wakati waliofaulu walikuwa wanafunzi 45,217 (sawa na asilimia 89.64), idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa wanafunzi 10,048, hata hivyo asilimia ya ufaulu imepungua kidogo kwa asilimia 0.78 mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam, katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani(Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 45,217 sawa na asilimia 93.76 ya waliofanya mtihani; wasichana waliofaulu ni 17,905 sawa na asilimia 94.07 na wavulana ni 27,320 sawa na asilimia 93.56. Imeandikwa na Boniface Meena. SOURCE: Mwananchi.

Ngoma za asili


Kikundi cha ngoma za asili cha Simba wa Vita wakitumbuiza kwenye maadhimisho ya kupiga vita ugonjwa wa saratani ya matiti yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Michael Jamson

President Kikwete attends the 3rd EAC Conference on Investment in Kampala


Some East African Heads of State and representatives of Heads of State who participated in the 3rd East African Community Conference on Investment held at Kampala Uganda pose for a group photograph with some members of their delegation.From left Rwanda's Prime Minister Bernard Makuza,Uganda's President Yoweri Kaguta Museveni,President Jakaya Mrisho Kikwete, Burundi's Vice President Dr.Yves Sahinguvu and Kenya's Prime Minister Raila Odinga
a cross section some participants to the 3rd EAC Conference on investment held at the Munyonyo Resort in Kampala.

The Secretary General for the East African Community ambassador Juma Mwapachu consults with the Chairman of the EAC Heads of State Summit President Jakaya Mrisho Kikwete during the closing sesssion for the 3rd EAC conference on investment held in Kampala this afternoon.Others from left President Museveni of Uganda,Kenya's Prime minister Raila Odinga and Rwanda's Prime Minister Bernard Makuza.

From left The Chairman of the East African Community Heads of State Summit President Jakaya Mrisho Kikwete, the host President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda and Kenya's Prime Minister Raila Odinga hold an informal discussion shortly before the conclusion of the 3rd East African Conference on Investment held at Munyonyo Speke Resort in Kampala this afternoon.

President Jakaya mrisho Kikwete delivers his speech during the closing session of the 3rd EAC Conference on Investment held in Kamapala(photos by Freddy Maro)

Thursday, April 29, 2010

Inaugural “Origin Africa Designer Showcase”








Robi Morro and Jamilla Vera Swai launch their Ready to wear collection

Inaugural “Origin Africa Designer Showcase” was held last night on 28 April 2010 in Nairobi at the Laico Regency which saw two Tanzanian Swahili Fashion Week designers Robi Morro and Jamilla Vera Swai Launch their new collection.

Tanzania Cotton Board’s (TCB) Textile Sector Development Unit (TSDU) – through the
Organisers’ of the Swahili Fashion Week – had facilitated the participation of Robi Morro and Jamilla Vera Swai.

The work of the Textile Sector Development Unit has been made possible by support from the Gatsby Charitable Foundation and its associated Tanzania Gatsby Trust (TGT). Tanzania Cotton Board wants to ensure that more Tanzanian grown cotton is transformed into higher value added products in Tanzania

Robi Morro of Mapozi Designs collection is named Garden of Style , which is inspired by the woman.” A woman is like a flower, she blossom well if taken good care of” said Robi. “The pieces are very feminine, flirty, sassy colourful and fun aimed at bringing out the woman's beauty with the use of bold colourful floral prints.” added Ms Morro

Jamila’s Collection is named “Say and Color Zero” Inspired by her daughter of two first school homework “Say and Color Zero”. This became her constant routine for every evening. “Her favourite colors being red and black, I decided working with that by layering them by individual colors, with the print zero” said Jamilla.

CONTACT PERSON: Mr. Mustafa Hassanali
TELEPHONE NUMBER: +255-78-4303880
EMAIL ADDRESS: media@swahilifashionweek.com
WEBSITE URL: http://www.swahilifashionweek.com

Ajali mbaya::WANAFUNZI 18 WAFA, 125 WAJERUHIWA


Wahudumu wa hospitali ya Bombo wakimpeleka majeruhi katika chumba cha upasuaji baada ya kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuwa wakitokea kwenye Maulid yaliyofanyika Kijiji cha Kibafuta kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Tanga na Mkinga jumla ya umla ya wanafunzi 18 walikufa na wengine 125 walijeruhiwa.

Mmoja wa majeruhi akiwa chini ya uangalizi wa daktari mtaalamu kutoka nje ya nchi majeruhi huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana alipata ajali baada gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuakiwa katika wodi ya Galanosi Hospitali ya Bombo baada ya gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuwa wakitokea kwenye Maulid yaliyofanyika Kijiji cha Kibafuta kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Tanga na Mkinga jumla ya umla ya wanafunzi 18 walikufa na wengine 125 walijeruhiwa.

Majeruhi Ali Maulid akiwa katika wodi ya Galanosi Hospitali ya Bombo baada ya gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuwa wakitokea kwenye Maulid yaliyofanyika Kijiji cha Kibafuta kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Tanga na Mkinga jumla ya umla ya wanafunzi 18 walikufa na wengine 125 walijeruhiwa. Imeandikwa na Burhan Yakubu.

*********************************************************

JIJI la Tanga limfeunikwa na simamzi kuu kufatia wanafunzi 18 wa Chuo cha Kiislamu cha Shamsil-Maariff kufa papo hapo na wengine 125 kujeruhiwa vibaya, baada ya lori walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye sherehe za maulidi kupinduka.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Adolphina Kapufi aliliambia gazeti hli jana kuwa ajali hiyo ilitokea saa 5:30 usiku wa kuamkia jana katika eneo la njiapanda kuu ya Mabanda ya Papa jijini hapa.

Kapufi aliwataja baadhi ya waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Twalib Kunemu, Juma Idd, Faraji Habib, Jahshi Rashid, Hussein Bakari, Hajji Athumani naYussuph Hussein na kwamba, kazi ya kuwatambua maiti wengine bado inaendelea.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Paschal Kanyinyi alisema kazi ya kuwatambua waliokufa na majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo wodi ya Galanosi inaendelea.

Kanyinyi aliwataja majeruhi waliotambuliwa kuwa ni Jumaa Salim ambaye ameumia mbavu, Makame Ahmed, Ahmed Shehe, Selemani Said na Juma Akida.

Aliwataja majeruhi ambao hali zao ni mbaya, hivyo waliokimbizwa katika Hospitali Taifa ya Muhimbili, jijini Dar essalaam kuwa ni Hemed Shaaban na Hassan Adam.

Kanyinyi alifahamisha kuwa kati majeruhi 125 walifikishwa katika hospitali hiyo usiku wa kuamkia jana baada ya kupata ajali, 70 walipata matibabu na kuruhusiwa kurejea chuoni kwao.

Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu huyo, majeruhi 55 wanaendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo kwa msaada wa timu maalumu ya waganga na wauguzi waliokusanywa kutoka hospitali na vituo mbalimbali vya afya mkoani Tanga kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.

Mwananchi ilifika katika Hospitali hiyo ya Bombo na kukuta idadi kubwa ya wananchi waliokusanyika katika hospitali hiyo kwa lengo la kutambua miili ya waliokufa na majeruhi.

Mwalimu wa zamu wa Chuo hicho, Ustaadh Ajali Ramadhan, alisema kuwa wanafunzi hao walikuwa wakitokea Kijiji cha Kibafuta ambako walikwenda kuhudhuria sherehe za kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W.

Ziara ya Waziri Mkuu


Mwanamke wa kijiji cha Msungua wilayani Singida (jina halikupatikana) akifurahia hotuba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa huo, Aprili 28, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza na Sister Maria Tesha wa Kituo cha Masister wa Kanisa Katoliki cha Ursula cha Mkiwa wilayani Singidaambako ameambatana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda anayeendelea na Ziara ya Mkoa huo, Aprili 28, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, April 26, 2010

MUUNGANO: Mkapa, Mwinyi wang'ara







UWANJA wa Uhuru leo ulifurika maelfu ya watu walioenda kushuhudia sherehe za maadhimisho ya Miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hisia za umati huo zilionekana wakati marais wastaafu, Ali Hassani Mwinyi na Benjamini Mkapa walipoingia.
Umati huo ulilipuka shangwe za kelele na vifijo wakati viongozi hao walipoingia kwenye uwanja huo mkongwe kwa nyakati tofauti kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuingia na kuzunguka uwanja mzima akipunga mkono.
Mkapa, ambaye aliongoza serikali ya awamu ya tatu ambayo ilijipatia sifa ya kuinua uchumi na kuboresha miundombinu, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia uwanjani katika siku hiyo iliyokuwa na jua la vipindi.
Baada ya Mkapa, ambaye aliongoza nchi kwa sera aliyoiita ya "ukweli na uwazi", kuingia uwanjani hapo kwa gari la kifahari aina ya Range Rover (Vogue), kelela za shangwe na vigelegele zililipuka kutoka kwenye umati wa watu.
Mkapa aliyeingia uwanjani hapo majira ya saa 3:15 alipishana kwa takriban dakika 15 na kiongozi wa serikali ya awamu ya pili, Mwinyi ambaye pia aliamsha kelele za shangwe kutoka kwa watu waliohudhuria.
Kama ilivyokuwa kwa Mkapa, Mwinyi ambaye aliingia uwanjani hapo na gari aina ya Toyota Landcruiser (VX) alishangiliwa kwa nguvu tofauti na ilivyokuwa kwa viongozi wa serikali ya sasa, akiwemo Rais Kikwete.
Shangwe kwa viongozi hao zilirindima kutoka jukwaa la kijani ambalo lilikuwa limepambwa na watu waliokuwa wamevalia fulana na kofia zenye rangi ya bendera ya taifa la Tanzania.
Mkapa amekuwa hajitokezi hadharani mara kwa mara na wakati mwingine amekuwa akikosekana kwenye sherehe kubwa kama maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika.
Kutoonekana kwake hadharani kumekuwa kukitafsiriwa kuwa kunatokana na kuandamwa na tuhuma za ufisadi kwenye serikali yake, zikiwemo tuhuma dhidi yake za kufanya biashara akiwa Ikulu.
Mkapa, ambaye alifanikiwa kukusanya kodi na kulipa madeni yaliyosababisha wahisani kuisamehe nchi, amekuwa hajibu tuhuma hizo na mara ya mwisho alisema: "Siwezi kuzuia masikio yenu kusikia, lakini naweza kuuzuia mdomo wangu kusema."
Mwinyi, ambaye pia aliwahi kuwa rais wa Zanzibar, aliongoza nchi enzi za mageuzi ya kiuchumi na kisiasa na kujipatia jina la Mzee wa Ruksa.
Imeandikwa na Sadick Mtulya na Patricia Kimelemeta. SOURCE: MWANANCHI


&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Malaria yamgeuka Afande Sele





UGONJWA wa malaria umemgeukia mwanaharakati wa kupinga ugonjwa huo kupitia muziki nchini, Afande Sele hadi kulazwa katika hospitali binafsi ya Mashuda iliyopo maeneo ya Mwananyamala A, wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Afande Sele ambaye ni mfalme wa rhymes nchini alihjikuta akikumbwa na ugonjwa huo licha ya kujiandaa vyema kufanya onyesho la mfano la kupinga ugonjwa huo katika tamasha lililofanyika katika vfiwanja vya mmnazi mmoja jijini hapo.
Akizungumza na Mwananchi akiwa amelazwa katika hospitali hiyo huku akiwa ametundikiwa dripu la tatu la kwinini, Afande Sele alisema ugonjwa huo ulimuanza bila kujijua mara tu baada ya kufika jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita majira ya usiku ambapo alihisi kuumwa na tumbo.
“Nilikuwa nimeshafika Dar baadaye kidogo nikajisikia tumbo linauma na muda ulivyozidi kwenda lilizidi kuuma nikaamua kwenda kupima ndipo nikakutwa na malaria iliyoanzia tumboni ndipo nilipoanza matibabu baada ya kulazwa katika zahanati hiyo,’’ alisema Afande Sele.
Afande alisema hadi asubuhi ya saa mbili ya siku ya maadhimisho ya tamasha la malaria alikuwa amekwisha maliza dripu tatu za dawa hiyo, ambapo alilazimika kuomba ruhusa na kwenda kufanya onyesho huku akiumwa marelia.
“Unajua umuhimu wa tamasha la lo imenilazimu kuomba ruhusa kwa dakika kadhaa nikaenda kupafomu na kisha nikarudi kumalizia dripu la tatu ambalo ndilo la mwisho alisema afande,’’ alisema Afand Sele
Hata hivyo tamasha hilo lilifana kwa kupambwa na wasanii mbalimbali akiwemo Afande Sele, Profesa Jay, Banana Zoro na wasanii kutoka THT.
Naye Waziri wa Afya, Profesa Mwakyusa alisema watu wengi wanaugua malaria kwa kuwa hawajingi na mbu waendezao ugonjwa huo na wengine hawachukui hatua za kuwakinga watoto wadogo ili wasipatwe na ugonjwa huo. Hata hivyo waziri huyo alisema Serikali inampango wa miaka mitano wa kuondoa ugonjwa huo hadi ifikapo mwaka 2015 ambapo zaidia ya 50 inatarajiwa kufikiwa. Imeandikwa na Festo Polea; SOURCE: MWANANCHI

Sunday, April 25, 2010

Jk amcheki Mbunge Kimaro


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jana asubuhi na Mbunge wa Vunjo(CCM) Aloyce Kimaro alyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kuugua shinikizo la damu juzi akiwa bungeni mjini Dodoma. (Picha na Freddy Maro)

Miss Universe Tanzania 2010




Miss Universe Tanzania 2010, Hellen Dausen akiwa na taji lake la maua alilopewa baada ya kutangazwa mshindi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha mabinti 20, mashindano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Ijumaa Usiku. Picha na Fidelis Felix.

Thursday, April 22, 2010

Kesi ya Miss Tanzania Miriam yafutwa


KESI ya kushambulia na kuharibu mali iliyokuwa inamkabili Miss Tanzania, Miriam Gerard, pamoja na rafiki yake imefutwa na wawili hao pamoja na mtu wanae shitakiana nae sasa watamalizana nje ya mahakama.
Uamuzi huo umefikiwa jana katika Mahakama ya Kinondoni ambako kesi hiyo ilifikishwa mwezi Februari.

Juan Antonio Samaranch hatunaye tena


Juan Antonio Samaranch (1920 - 2010)
Dunia na hasa ulimwenguwa michezo umempoteza mtu mashuhuri sana, aliyekuwa raisi wa Kamati ya Olimpiki duniani (I.O.C) bwana Juan Antonio Samaranch, ambaye amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 89.

Bwana Samaranch anakumbukwa kwa kuchukua uongozi wa IOC kutoka kwenye kipindi kigumu cha migomo toka nchi mbalimbali na matatizo ya kifedha kiasi cha kutishia kufilisikakwa shirikisho hilo.

Alipoingia madarakani mwaka 1980, bwana Samaranch alibuni na kufanikisha miradi kadhaa ya kuliingizia fedha katika Shirikisho hilo, kiasi cha kulianya kuwa shirika lenye utajiri wa kibilionea. Alitengeneza faida ya dola za Kimarekani milioni mia mbili na hamsini ($250,000,000) kutoka dola laki mbili tu ($200,000) alizozikuta alipoingia madarakani.
Habari kamili. KWA HABARI ZA KINA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI HEBU TEMBELEA hapa

Wednesday, April 21, 2010

Exim bank yatangaza mafanikio


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Mrs. Sabetha Mwambeja (kati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maendeleo ya benki yake, ikiwa ni pamoja na kusambaza huduma mikoani na visiwani Zanzibar. Kulia ni Meneja Mkuu wa Benki hiyo Dinesh Arora. Photo/ Fidelis felix

Tanzia

Mzee wa Mshitu na familia yake wanasikitika kutangaza kifo cha kaka yao, Rubani na Meja wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Hussein Charahani, aliyefariki Dunia usiku wa kuamkia Jumanne ya April 13, 2010 katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam na amezikwa nyumbani Nachingwea Aprili, 16 mwaka huu. Alikuwa rubani mahiri wa ndege za kijeshi na mtu mwenye kutegemewa sana katika Jeshi na pia familia yake.
Mola ailaze roho yake mahala pema peponi. Amina.
Kwa Habari zaidi

Sunday, April 11, 2010

RAIS WA POLAND NA MKEWE WAFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE


RAIS wa Poland Lech Kaczynski (pichani) na mkewe Maria na Mkuu wa Majeshi, Franciszek Gagor wamefariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea kusini mwa Smolensk.
Maofisa wa jimbo hilo walisema jana kuwa, katika ajali hiyo pia walikuwemo maofisa kadhaa wa serikali yake, akiwemo Gavana wa Benki Kuu, Slawomir Skrzypek na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Andrzej Kremer.
Walisema kuwa hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo iliyotokea wakati ndege hiyo ilipogonga miti ilipokuwa ikitaka kutua.
Maofisa hao walisema, tukio hilo lilisababishwa na hali mbaya ya hewa iliyotokana na ukungu kutanda katika sehemu mbalimbali za jimbo hilo.
Maofisa hao waliku wakienda Russia katika sherehe za kuadhimisha miaka 70, tangu kumalizika kwa mauaji ya Katyn. Sherehe hizo huadhimishwa kutokana na mauaji ya halaiki ya polisi zaidi ya 20,000 wa Poland.
Mauaji hayo yalifanywa na polisi maalumu wa iliyokuwa Jamhuri ya Muungano wa Kisovieti wakati wa vita vya pili duniani.
Tukio hilo limewaacha Wapoland katika majonzi, ikizingatiwa kwamba serikali ya Rais Kaczynski imefanikiwa kudhibiti hali ya kisiasa na kiuchumi katika taifa hilo.
Habari kutoka Warsaw, Poland zilisema Waziri Mkuu Donald Tusk alikuwa katika hali ngumu baada ya kupewa taarifa za msiba huo. Kiongozi huyo alishindwa kuzungumza chochote na alionekana akilia kwa uchungu.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa Russia, Irina Andrianova alisema ndege hiyo ilikuwa ikitokea Moscow kwenda Smolensk, na kwamba haikuwa na matatizo yoyote wakati ilipoondoka.
Naye Gavana wa Smolensk, Sergei Antufiev alikaririwa na kituo cha televisheni cha Russian akisema hakukuwa na dalili za uhai katika eneo la tukio.
" Wakati ikijiandaa kutua, ndege hiyo ya Rais haikufanikiwa. Taarifa za awali zinaonyesha kwamba iligonga miti, ikaanguka chini na kusambaa katika vipande. Hakuna mtu aliyenusurika.
“Kwa sasa tunafuatilia kujua (ndani ya ndege hiyo) kulikuwa na ujumbe wa watu wangapi. Taarifa zinadai walikuwa 85, “ alisema gavana huyo. Hata hivyo, wachunguzi wa Russia walidai kulikuwa na maofisa 132.
Kaczynski alichaguliwa kuwa Rais mwaka 2005 na kabla ya hapo alikuwa Meya wa mji wa Warsaw kwa miaka mitatu.

Thursday, April 08, 2010

NEC yaibuka na mambozz


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Chipukizi wakati akienda kusalimiana na wananchi na wajumbe wa mkutano huo wa NEC, alipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kuendesha kikao hicho.

Mambo ya mashujaa Musica


Salha Salehe

Salha Salehe, Rose, Masaki

Amosi Solo

Elystone Angai

Mariam+Lela+Pee

Bendi Mpya ya Mashujaa Musica ambayo imeundwa mwaka huu na kuweza kufikia mafanikio makubwa kwa muda mfupi hata kufikia kuliteka jiji la Dar es Salaam na Vitongoji vyake baada ya kuteremsha vibao viwili ambavyo mashabiki kote nchini waliobahatika kusikia na kutazama katika televisheni wameweza kushuhudia jinsi bendi hiyo inavyokuja kwa kasi hata kuwaweka roho juu baadhi ya wamiliki wa bendi kubwa zikiwemo za Twanga, Fm Academia na Acudo Impact.

Mashujaa Musica kwa sasa ipo chini ya uongozi wa Elystone Angai anayesaidiwa na Jado Fidifosi makao makuu yake yakiwa ni Eneo la Vingunguti Kiembe Mbuzi, ambapo Ukumbi wake wa Nyumbani ukiwa ni Mashujaa Pub uliopo katikati ya Vingunguti.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Mamaa Sakina (Cash Lady), amewapongeza kutokana na mwenendo mzuri wa sanaa yao ambayo anasema wakiendelea hivyo wataweza kufika mbali ikiwa ni pamoja na kujipatia kipato na kuweza kujitangaza wao wenyewe kimuziki.

“Ni kinyume na matarajio yetu kwani hatukutarajia kama wasanii hawa wanauwezo mkubwa kiasi hiki ambapo kama unavyosikia tangu waunde kundi hili la Mashujaa pamoja na kwamba ni muda mfupi lakini kazi zao zimeendelea kuonekana ikiwa ni pamoja na kusikiwa katika vituo mbalimbali vya Radio, na kazi zao zimeonekana ni wabunifu wazuri wa masuala ya muziki,”alisema Mamaa Sakina.

Aidha amewasifu kwa utulivu walioonyesha tangu walipoweza kujiunga na kampuni hiyo kwa lengo la kufanya kazi wakiwa kama wanamuziki, ambapo mpaka sasa tayari wameshafanikiwa kurekodi nyimbo mbili ambazo ni Moshi wa Sigara na Mwanike huku wakiwa Studio kukamilisha Wimbo wa Safari yenye Vikwazo unaoonekana kuja kutikisa Dunia kutokana na jinsi wimbo huo ulivyobeba hisia nyingi.

Mmoja wa wanenguaji wake, Mariam Leila pee ambaye kwa sasa ndiye mnenguaji mahiri, anazungumzia historia yake kwamba alitokea Tamaling iliyokuwa Zanzibar kabla ya kuibukia Acudo Impact, Diamond Musica, Vijana Classic kwa sasa anapigiga kazi yake na mashabiki wameikubali mashujaa Musica, na anawambiwa wapenzi wake anaipenda mashujaa kutokana naanakubali kazi ya mashujaa ni ya kimataifa siyo ya kitaifa,

“Mkae mkao wa kula kuangalia kazi ya mashujaa na wanenguaji wa mashujaa na kusikiliza muziki wa ukweli na magitaa ya ukweli kutoka kwa Kiongozi wa kundi Elyston Angai, hatuna mpinzani sisi ni mwanzo na mwisho, tunawapenda sana wapenzi wetu, na mimi kama Leila Pee sijawahi kuona mziki kama mashujaa Big Up Elyston Angai, Jado Fidifosi, Baba Isayan (Chochea), ambao mnafanya kazi kubwa viongozi wangu bendi ya mashujaa Intertainment- Mamaa Sakina, Papaa Maisha, Papaa Yohana, tuko tayari kufanya kazi kwa moyo mmoja hapa kazi tuu Kolala Tee” anasema Leila Pee.

Ni mzaliwa pekee yake kutoka kwa mama Fatma-mkazi wa Dar es Salaam yeye akiwa ni mtoto wa kwanza na mwisho kuzaliwa katika familia yake, ikiwa a maana ni mzaliwa pekee katika tumbo la Fatma mwaka 1984 mwezi wa sita katika hospitali ya Amana jiji Dar es Salaam.

Akizungungumzia historia yake Leila Pee anasema alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Kijichi iliyoko katika Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es Salaam alianza kuipenda fani ya muziki tangu akiwa mdogo, alipokuwa akisikia nyimbo za wanamuziki Gato wa nchini Congo, aliyeimba (hazarakise hawaa,) Mwanamuziki Madilu System(Mamuu) ndipo alianza kama mchezo, wakati huo alianza kucheza kwa watu, zinapopigwa nyimbo hizo, na zaidi anasema anakumbuka jinsi Dogodogo Rashidi alivyoweza kumsaidia kipindi hicho kuhusu kazi yake mpaka hatua aliyofikia.

Kwa upande wa Salha yeye ni mzaliwa wa tisa wa familia ya Mzee Salehe Athumani -mkazi wa Kipawa yeye akiwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa (kitinda mimba) katika tumbo la Zainabu Ibrahim mama mzazi wa Salha miaka 23 iliyopita tangu kuzaliwa kwake mwaka 1987 kwenye hospitali ya Amana iliyopo jijini Dar es Salaam.

Akiwa ni mtoto wa kike wa sita tangu wenzake kutoka tumboni mwa mama yao kuzaliwa, kabla ya kupendwa na mwenyezi Mungu (aziweke roho zao mahali pema peponi-akina Mariam Salehe, Zulfa Salehe, Sophia Salehe, na Amina Salehe), Salha anasema kuwa ndugu zake hao baada ya kufariki, alibaki mpweke kitendo kilichomfanya pia ashindwe kuendelea na masomo kutokana na familia yake kutokuwa na uwezo.

Kwa sasa Salha anasema wamebaki watoto watano wa kike wakiwa ni wawili yeye ya Idayab Sarehe, pamoja na kaka zao Jafari Sarehe, Isiaka Sarehe, na Abubakari Sarehe ambao mpaka sasa wapo wakiendelea kuishi nyumba ya Familia yaani ya Mzee Sarehe Athumani .

Akizungungumzia historia yake Salha Salehe anasema kuwa, alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Kipawa ambayo ipo katika wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam na alifanikiwa kumaliza shule ya Msingi mwaka 2002 bahati mbaya ama nzuri kwake hakuweza kuendelea na masomo kutokana na kuipenda sana fani ya muziki ambapo moja kwa moja alianza safari yake kuelekea katika suala zima la Muziki.

Wednesday, April 07, 2010

Rais kikwete ahudhuria Karume Day Zanzibar



Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Watano kulia) Rais Wa Zanzibar Amani Abeid Karume (Wasita kulia),pamoja viongozi wengine wa kitaifa wakiomba dua katika kaburi la muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Hayati Mzee Abeid Amani Karume huko katika ofisi kuu ya CCm Kisiwandui Zanzibar leo asubuhi.wengine katika picha kutoka kushoto Naibu Waziri kiongozi wa SMZ Ali Juma Shamuhuna,Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar Salehe Ramadhani Feruzi,Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha, na makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete(wanne kushoto) na Rais Amani Abeid Karume wakiwa katika ibada maalumu ya kumkumbuka muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Mzee Abeid Amani Karume iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM Kiswandui Zanzibar leo asubuhi.Wengine katika picha kutoka kushoto ni spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Naibu Waziri kiongozi wa SMZ Bwana Ali Juma Shamhuna, Naibu Katibu kuu wa CCM Zanzibar Salehe Ramadhani Feruzi,Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein(Wa saba kushoto),Waziri Kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha,Waziri Kiongozi Mstaafu wa SMZ Mohamed Gharib Bilal na Katibu Mkuu wa CUF Seif Shariff Hamad.

Maghorofa mapya ya Michenzani


MAGHOROFA MICHENZANI YANAVYOONEKANA SASA

ZAMANI ILIKUWA HIVI
Maghorofa mpya yaliyopo mtaa wa Michenzani Zanzibar yaliyoanza kujengwa kwaajili ya makazi bora ya Wananchi wa Zanzibar na hayati Mzee Abeid Amani Karume na kukamilishwa na Rais wa sasa Amani Abeid Karume.Makazi hayo tayari yamenza kugawanywa kwa wananchi waliokusudiwa kwa utaratibu maalumu(picha na Freddy Maro)

Kitu movie Bwagamoyo


Hello,

Welcome to another weekend of arts and entertainment at TaSUBa Theatre in Bagamoyo, We appreciate your help in making this known among your staff, friends and co-workers.


Thursday 8th April: African Film titled FINYE (THE WIND), at 8 pm

Friday 9th April: Starlight Disco with Dj Nature and Friends at 8 pm

Saturday 10th April: Bagamoyo Talents with different artists from Bagamoyo performing Live Music, Drama and Dance from 8 pm, plus Disco.


With kind regards from
Kjetil Haugbro
TaSUBa Theatre

Tel: 0769070814

Tuesday, April 06, 2010

Rais Kikwete apindua maamuzi ya UWT

RAIS Jakaya Kikwete amepindua maamuzi ya UWT walimbwaga Husna Mwilima, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT), kwa kashfa na kejeli wakidai hafai, sasa Mwilima ameula na anakuwa DC mpya wa Tandahimba wakati huo huo amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya nchini kwa kuwahamisha na kuwapangia vituo vipya kama ifuatavyo:-

1. Gishuli M. Mbegesi - Njombe amepangiwa kwenda Kilindi
2. Leonidas T. Gama - Mbeya amepangiwa kwenda Ilala
3. Frank A. Uhaula - Tarime ameoangiwa kwenda Kiteto
4. Bi. Sarah Dumba - Kilindi amepangiwa kwenda Njombe
5. John B. Henjewele - Kiteto amepangiwa kwenda Tarime
6. Rashid M. Ndaile - Chunya amepangiwa kwenda Mkinga
7. Evans Balama - Ilala amepangiwa kwenda Mbeya
8.Florence A. Horombe -Bukombe amepangiwa kwenda Nzega
9. Bi. Zainab Kwikwega -Kasulu amepangiwa kwenda Makete
10. Bi. Hawa Ngh’umbi -Makete amepangiwa kwenda Bukombe
11. Lt. Col. John Mzurikwao -Mpanda amepangiwa kwenda Sumbawanga
12. Bi Betty Machangu -Nzega amepangiwa kwenda Kasulu
13. Dk. Rajab Lutengwe -Ulanga amepangiwa kwenda Mpanda
14. Francis Miti -Tandahimba amepangiwa kwenda Ulanga
15. Deodatus Kinawiro -Mkinga amepangiwa kwenda Chunya

Taarifa ya uteuzi huo iliyosainiwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bw. Aggrey Mwanri imesema pamoja na mabadiliko hayo, Rais Kikwete pia amemteua Bibi Husna Mwilima aliekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Wanawake kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba kuchukua nafasi ya Ndugu Francis Miti ambaye anahamia wilaya ya Ulanga.

Aidha, Rais Kikwete ametengua uteuzi wa Bw. Thobias M. Sijabaje ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kutokana na kutosimamia vizuri zoezi la ugawaji wa vocha za pembejeo za kilimo katika wilaya ya Sumbawanga katika msimu wa mwaka 2009/2010.

Mabadiliko haya yanakusudia kuongeza ufanisi wa kazi, kuimarisha utendaji katika wilaya hizo na yanaanza mara moja.


Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S. L. P. 3021
DAR ES SALAAM
Jumanne, Aprili 06, 2010.

Wanafunzi wabongo waula Marekani


Five Tanzanian youths and one secondary school teacher before they departed for the United States for a four-week Youth Leadership Exchange Program (March 27 - April 21). The students will live with local hosts' families in Washington D.C. and Denver, Colorado and interact with U.S. teenagers, grassroots activists and community organizations. The American people are sponsoring this program to give Tanzanian students an opportunity to learn more about the rights and responsibilities of all citizens in a democracy. This is the second group of Tanzanian youth to participate in the Youth Leadership Exchange Program in the past six months. U.S. Embassy Deputy Public Affairs Officer Karen Grissette is third from left. (Photo courtesy of the American Embassy)

Usafiri wa Kusini


Magari yakiwa yamekwama kwenye tope eneo la Kiwanga mkoani Pwani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini na kusababisha usumbufu kwa wasafiri. Magari hayo yalikuwa yakitokea Dares Salaam na mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara yalikwama kwa siku mbili. (Picha na Exuper Kachenje)

Monday, April 05, 2010

Wahamiaji haramu


Wahamiaji kharamu kutoka nchini Somalia wakipandishwa kwenye gari la polisi mara baada ya kukamatwa wakiwa katika kisiwa cha Songo Mnara ambako walitelekezwa na manahodha wa boti waliyokuwa wakisafiria baada ya kuwadanganya kuwa wameshafika Msumbiji walikokuwa wakielekea jumla ya wahamiaji 67 walikamatwa. Picha na Said Powa

Breaking Newwssss:: Mwandishi mkongwe Konga afariki Dunia

MWANDISHI wa habari mkongwe na mchambuzi wa masuala ya siasa, jamii na utawala, Aristariko Konga amefariki dunia.

Taarifa zilizopatikana jana hospitalini Lugalo alikokuwa amelazwa takribani wiki mbili zilizopita zilieleza kuwa Konga alifariki dunia jana majira ya saa kumi jioni baada ya hali yake ya kiafya kubadilika ghafla.

Akizungumza na Mwananchi, Shemeji ya marehemu Konga, Godlove Ndingala alisema kuwa shemeji yake alifariki dunia jana jioni baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda.

"Ndugu yangu ni kweli yametufika, shemeji Konga ameaga dunia majira ya saa kumi hivi, hapa unapozungumza na mimi ni dakika chache tumetoka kupata uthibitisho wa kitabibu kuhusiana na kifo hicho,"alisema.

Alisema mipango zaidi ya mazishi ya marehemu Konga inafanyika, lakini kwa sasa msiba utakuwapo nyumbani kwa marehemu eneo la Ubungo Kibo karibu na baa ijulikanayo kama Kipembele.

"Kikao cha familia bado hakijakaa, lakini kwa kuanzia ni kwamba msiba utakuwapo nyumbani kwake kule Ubungo Kibo,"alisema Ndingala.

Historia ya Konga si nyepesi kuielezea, lakini amepata kuwa mwandishi na Mhariri Mwandamizi wa kampuni zinazochapisha magazeti ya Mwanahalisi, Mwananchi, Raia Mwema na The Guardian.

Konga atakumbukwa kwa ujasiri wake katika kusimamia mambo ya msingi kwani wakati fulani aliunguliwa nyumba katika mazingira ya kutatanisha suala ambalo lilidhaniwa kuwa uunguaji huo ulikuwa ni shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya msimamo wa gazeti hilo katika masuala kadhaa ya kitaifa.

Nyumba iliungua na kuteketeza mali zote isipokuwa godoro na kitanda vilivyokuwa katika chumba cha watoto kilichonusurika, na zaidi Konga alibakiwa na suruali mbili na shati moja zilizokuwa zimeanikwa katika kamba nje ya nyumba baada ya kufuliwa.Konga ameacha mke na watoto kadhaa. Kwa hakika medani ya habari imepata pigo. SOURCE: MWANANCHI

Jumatatu ya Pasaka


WAUMINI WA KANISA KATOLIKI ZANZIBAR WAKITOKA NJE BAADA YA KUMALIZA KUSALI MISA YA JUMATATU YA PASAKA KWENYE KANISA LA MTAKATIFU JOSEFU MJINI ZANZIBAR.

WANAKWAYA YA MTAKATIFU JOSEFU,KANISA KATOLIKI ZANZIBAR WAKITUMBUIZA KWENYE MISA YA JUMATATU YA PASAKA LEO.

Mvua za masika zinazoendelea kunyesha Visiwani Zanzibar zimesababisha maeneo mengi kujaa maji, pichani barabara ya Ally Hassan Mwinyi inayoanzia Darajani hadi Mlandege ikionekana imefurika maji mengi kiasi cha kuwa kero kwa wenye maduka na wapita njia.
PICHA ZOTE NA MARTIN KABEMBA.