Tuesday, December 30, 2008

huu mchezo wa mafuta tumeuchoka



Pichani unaweza kumuona askari anayelinda kituo cha mafuta kinachodaiwa kufungwa kutokana na kukosa mafuta lakini waagizaji wakubwa wa mafuta nchini wamewakana wamiliki wa vituo vya kuuza nishati hiyo na kushangazwa na kitendo cha kupandisha bei kiholela wakati wa Sikukuu ya Krismasi kwa kisingizio cha uadimu wa mafuta baada ya meli kuzuiwa na maharamia wa Kisomali.

Kauli ya waagizaji hao imekuja siku moja baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima kueleza kuwa akiba ya mafuta iliyopo ni kubwa ya kuweza kutosheleza mwezi mzima na kushangazwa na hatua ya wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta kwa madai kuwa ni adimu.

Bei ya mafuta ilipanda ghafla usiku, siku moja kabla ya Krismasi huku baadhi ya vituo vikifungwa kwa maelezo kuwa kuongezeka kwa vitendo vya maharamia wa Kisomali kuteka meli za mizigo kwenye pwani ya Somalia kumefanya meli zilizobeba shehena za mafuta yanayokuja nchini kushindwa kupita na hivyo kusababisha uhaba wa nishati hiyo muhimu.

Monday, December 29, 2008

Kubenea akiwa na Paschal


MKURUGENZI Mtendaji wa gazeti la MwanaHALISI (ambalo liko kifungoni), Saed Kubenea mwenye miwani, akimjulia hali mwanahabari Pascal Mayala jana katika hospitari ya Apollo Indraprastha, mjini Delih nchini India.

Mayala amelazwa hopitari hapo akipata matibu yaliotokana na ajali ya pikipiki miezi mitatu iliyopita ambapo alijeruhiwa vibaya mguu wa kushoto, mkono wa kushoto na bega la kushoto.

Kwa upande wake, Kubenea yupo nchini India kwa takribani mwezi mmoja sasa, akipata matibabu ya macho yaliotokana na kuvamiwa na kumwagiwa tindikali, ofisini kwake Januari 05 mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PPR, Pascal Mayala akiwa amelazwa katika Hospitali ya Apollo Indraprastha, mjini Delhi nchini India anakotibiwa baada ya kujeruhiwa vibaya katika ajali ya pikipiki iliyotokea hivi karibuni nchini.

Picha na (mpiga maalum)

Friday, December 26, 2008

jamaa na mambo ya krismasi


Mkazi huyu wa mkoa wa Arusha alikutwa akiwa amelala ndani ya mtaro huku akiwa
hajitambui jirani na kituo kikuu cha polisi mkoani hapa.Wapita njia walisema kuwa
mtu huyo alikuwa amelala baada kunywa pombe akisherehekea sikukuu ya krismas.(picha
na Hemed Kivuyo)

Friday, December 19, 2008

Kijarida Cha Cheche Mitaani-Jinsi walivyoitafuna ATCL


Je ATCL imefikaje hapa hadi kujikuta inasimamisha huduma yake? Ni kwanini shirika la IATA liamue kuisimamisha ATCL? Je ni kweli tatizo la ATCL ni fedha! Umesikia kuhusu Dowans na jaribio lililofeli la kujaribu kuitengenezea mshiko licha ya kampuni hiyo kurithi mkataba usio halali wa Richmond?
Umewahi kusoma maoni ya Rev.Kishoka (Waumini wake wako kwenye mtandao!)? Vipi kuhusu hoja za nguvu zisizo na kigugumizi za mwanakijiji na mawazo ya kina ya Dada Jessy? Kama umejibu "hapana" kwenye swali lolote hapo juu basi wewe ni miongoni mwa watu ambao hawajapata nafasi ya kusoma kijarida cha bure, huru, na kinachotubutu zaidi cha "Cheche za Fikra". Unaweza kujisomea kwenye mtandao wa habari wa
http://www.forums.mwanakijiji.com/forumdisplay.php?f=62 au unaweza kujiandikisha kupata kijarida hicho kwenye email yako kila wiki kwa kuomba kutumiwa kijarida hicho kwa kutuma ombi la kuandikishwa kupitia klhnews@gmail.com
Na sisi tunaweza!
Twende na tuwe "Cheche"Mhariri!

Mgonja atoka lupango





Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Gray Mgonja, leo alifikishwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mbele ya Mheshimiwa Henzroni Mwankenja kushughulikia suala la dhamana ambalo ilifanikiwa baada ya mawakili wake kuwasilisha hati ya nyumba sita pamoja na Hati ya kusafiria ya mshitakiwa, pichani Mgonja akiwasalimia ndugu zake wakati akiingizwa mahakamani hapo.Picha za http://www.globalpublisherstz.com

Miss East Africa Bujumbura leo





Picha kwa mujibu wa Mpoki Bukuku

Herry Makange aagwa



Ndugu jamaa na marafiki wakimfariji mjane wa marehemu

KWA MUJIBU wa taarifa ambazo tumezipata Mwili wa Marehemu Herry Makange umeagwa leo hapa jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Mzee Mponzi ( Baba Mkwe wake) Oysterbay Mtaa wa Msasani nyumba N0 35 saa 6 hadi saa 8 mchana na baadae mwili wa Marehemu utasafirishwa hadi Kibaha Vigaeni nyumbani kwao kwa maazishi yatakayo fanyika huko huko Kibaha. (Picha ya Mrocky Mrocky)

Deus Malya ndani ya mahakama




Deus Malya (left) in consultations with his advocate Godfrey Wasong a.k.a White before the proceedings of a traffic case against him at the Dodoma Resident magistrate court yesterday. Photo/Jube Tranquilino

Thursday, December 18, 2008

Herry Makange afariki dunia




HAYATI HERRY MAKANGE

Habari tza kusikitisha tulizozipoke hivi punde kutoka kwa issamichuzi.blogspot.com zinasema kuwa HERRY MAKANGE, MPIGANAJI WA CHANNEL TEN NA DTV, HATUNAYE TENA BAADA YA KUFARIKI KATIKA AJALI HAPA DAR JANA MCHANA.

HABARI ZILIZOPATIKANA JANA USIKU NA KUTHIBITISHWA ASUBUHI HII NI KWAMBA HERRY ALIKUTWA NA MAUTI AKIELEKEA MJINI KUTOKEA KAWO KIBAHA AKIWA ANAENDESHA PIKIPIKI. ALIKUWA NDIO KWANZA AMEREJEA TOKA TABORA KIKAZI NA ALIKUWA AKIENDA KURIPOTI KAZINI.
IKUMBUKWE KWAMBA HERRY ALIKUWA MMOJA WA WAPIGANAJI WALIONUSURIKA KATIKA AJALI YA GARI HUKO KIBITI ILIYOMHUSISHA PIA MPIGANAJI ATHUMANI HAMISI AMBAYE HADI LEO YUKO SAUZI AKITIBIWA SHINGO NA MGONGO. KURASA YA AJALI HIYO YA KIBITI BOFYA HAPA
TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA KILA KINACHOJIRI BAADAYE IKIWA NI OAMOJA NA MIPANGO YA MAZISHI.
MUNGU AILAZE ROHO YA MPIGANAJI MWENZETU MAHALI PEMA PEPONI
-AMINA

Wednesday, December 10, 2008

Huduma za ndege ATCL zasitishwa ndani, nje ya nchi


Moja ya ndege za Shirika la Ndege Tanzania ambalo sasa huduma zake zimesimamishwa.

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL), ambalo limekuwa na matatizo makubwa tangu ndoa yake ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) ivunjike, limenyang’anywa cheti cha kuruka angani na Mamlaka ya Anga (TCAA) baada ya kukosa viwango vya ubora kuruka angani.

Taarifa kutoka ndani ya ya ATCL zimeeleza kuwa shirika hilo limenyang’anywa cheti hicho tangu Desemba 8 mwaka huu na hivyo litashindwa kusafirisha abiria hadi hapo litakapokidhi masharti ya usalama wa anga na kurejeshewa cheti hicho.

Miongoni mwa viwango hivyo vya usalama ni ukaguzi wa mara kwa mara wa ndege zake, kuwa na wataalamu wa kutosha kama marubani na wahandisi, vitu ambavyo vimeonekana kukosekana kwenye shirika hilo la serikali.

Kufungiwa huko kumekuja huku kukiwa na uwezekano wa shirika hilo kufungiwa na Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (IATA) kufanya safari zake baada ya kubaini zaidi ya makosa 500.

Mwishoni mwa wiki iliripotiwa kuwa ATCL ilikaguliwa mwezi Oktoba na kubainika na makosa hayo ya usafiri wa anga, lakini ikashindwa kuyarekebisha na ndipo IATA ilipoanza mchakato wa kutaka kuizuia kufanya safari.

“Ni kweli ATCL imenyang’anywa cheti cha viwango kwa kukosa ubora wa kuruka angani hivyo haitafanya safari za nje wala ndani ya nchi,” alisema mmoja wa watu wa ndani TCAA alipohojiwa na Mwananchi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ndege za ATCL zilizokuwa zikifanya safari zake ndani na nje ya nchi haitaweza kufanya tena safari hizo na vigogo wa ATCL jana walikuwa na vikao na TCAA kuzungumzia suala hilo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo alisema hana taarifa kuhusu kunyang’anywa cheti kwa ATCL na kudai kuwa mkurugenzi wa shirika hilo, David Mataka ndiye anayeweza kueleza suala hilo.

“Sina taarifa kuhusu suala hilo... hayo ni mambo ya ATCL na anayeweza kukueleza ni Mataka, hivyo wasiliana naye... haiwezekani toka tarehe nane hadi leo mimi sijui,” alisema Chambo.

Tuesday, December 09, 2008

Mchezo wa bao


Nimaarufu saana mchezo huu ukichezwa na watu wa rika mbalimbali na katika nyakati tofauti, ni mchezo wa kijadi na aliupendelea sana hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere, hebu cheki watoto sijui wanacheza au wanazuga!

Miaka 47 ya uhuru wa tanzania




MAMA Maria Nyerere na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, jana walikuwa kivutio katika maadhimisho ya Sherehe za Uhuru yaliyofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam baada ya kushangiliwa na umati wa watu waliohururia sherehe hizo huku viongozi wengine wakiingia kimya kimya.

Kitendo cha wananchi kuwashangilia viongozi hao kwa nderemo na vifijo bila hata kuhamasishwa ilileta utofauti mkubwa kati yao na Rais Jakaya Kikwete ambaye alishangiliwa na baadhi ya makundi hasa baada ya kutangaziwa na mwongoza sherehe.

Akitangaza wakati msafara wa rais unakaribia kuingia uwanjani huku watu wakiwa kimya, mwongoza sherehe huyo alisema: “Mabibi na mabwana tunayemtarajia kuingia uwanjani hivi sasa ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete, hivyo atakapoingia uwanjani ninaomba tumshangilie kwa nguvu zetu zote.”

Hata hivyo, muda mfupi baada ya tangazo hilo Rais Kikwete akaingia uwanjani kwa kutumia geti kubwa na kuzunguka uwanja akiwa katika gari la wazi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ndipo makundi hayo yakijaribu kushangilia kwa sauti ya chini huku baadhi yao wakipeperusha bendera ya Taifa.

Watoto bwana


Watoto wakiwa katika michezo yao bwana huwawezi ni ma expert wa michezo yao hebu wacheki hawa watoto wamebuni mchezo wao, hii ilikutwa na mdau wetu Juma Uledi wa Morogoro

Monday, December 01, 2008

Jupiter, Venus, mwezi zakutana


VITU vitatu jana vilikuwa viking'aa angani vikiwa vimejipanga pamoja; ni sayari za Jupite na Venus ambazo ziliuzunguka mwezi uliokuwa ukionekana kama mithili ya ukucha uliokatwa.

Ni tukio lisilo la kawaida kutokea, lakini hutokea kila baada ya miaka kadhaa. Baada ya tukio la jana, sayari hizo na mwezi zitakaribiana tena Novemba 18 mwaka 2052.

Jupiter na Venus zilianza kusogea kuelekea karibu na mwezi juzi jioni na ilipofika jana zilionekana zikiwa umbali wa digrii 2, ambazo ni sawa na kidole kilichonyooshwa kwenye mkono, anasema Alan MacRobert, mhariri mwandamizi wa jarida la Sky and Telescope alipoongea na AP.

Tofauti na hali inavyokuwa wakati jua likikamatwa na mwezi, jana haikuhitaji kiona mbali kushuhudia tukio hilo kutokana na vitu hivyo vitatu kutoa mwanga mkali, mwezi ukionekana kuwa mkubwa zaidi na kufuatiwa na Jupiter, ambayo ilionekana upande wa kushoto, huku Venus ikionekana kuwa ndogo kuliko zote.

Vibaka wawapa polisi kibarua kizito Mtoni Kizinga



Hebu cheki wananchi wa Mto Kizinga wanavyopata shida kuweza kupita kwenda au kurudi kutoka kwao Mbagala ni karaha kubwa mno, jana jeshi la polisi lilimwaga askari wake katika daraja la Mto Kizinga lililopo Mtongani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kudhibiti vibaka walioanza kutumia fursa ya adha ya kuvuka mto huo kuwapora watu mali zao.

Daraja la mto Kizinga limefunikwa na maji baada ya mvua kubwa iliyonyesha juzi maeneo ya Kisarawe hali ambayo imewalazimisha watu kuvuka mto huo kwa miguu baada ya magari kushindwa kupita.

Vibaka hao walikuwa wakijibanza pembeni mwa daraja hilo lilofunikwa na maji na kuwapora watu wanaopita eneo hilo kwa miguu vitu mbalimbali na kusababisha uvunjifu wa amani.

Polisi hao wamemwagwa eneo hilo baada ya malalamiko kadhaa ya watumiaji wa njia hiyo kutaka polisi wadhibiti vitendo hivyo kwa ulinzi wa silaha.

“Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana katika daraja hili tulikuwa hatupiti kwa raha yaani Jana na juzi ikifika saa moja asubuhi au jioni hujavuka katika daraja hili basi ujue lazima utakabwa,” alisema Irene John wakati akiongea na Mwananchi na kuongeza kuwa

“Jana mama mmoja alikuwa akipita eneo hili alipigwa na kuporwa pochi pamoja na simu na vibaka na polisi walifika mara moja na kumkamata tunashukuru kwani polisi wamefika na hali ni shwari kabisa hakuna tena matukio ya uporaji” . Habari imeandikwa na Christina Kabadi.

Friday, November 28, 2008

Barabara



Picha ya kwanza ni mto unaokatisha barabara ya kuunganisha kijiji cha Uwiro na Ngerenanyuki wilayani Arumeru ukiwa umejaa maji na hivyo kusababisha kero kubwa kwa wakazi wa kata ya Ngarenanyuki kutokana na kutokuwa na daraja kwa miaka mingi sasa. picha na Mussa Juma

Thursday, November 27, 2008

ADB imemwaga bilion 192.9/- kwa ajili ya bajeti


Treasury Permanent Secretary Gray Mgonja exchanges documents with African Development Bank Resident Representative Ms Sipho Moyo after signing 192.9 billion Tshs for the General Budget Support in Dar es Salaam today.

ADB imemwaga bilion 192.9/- kwa ajili ya bajeti


Treasury Permanent Secretary Gray Mgonja exchanges documents with African Development Bank Resident Representative Ms Sipho Moyo after signing 192.9 billion Tshs for the General Budget Support in Dar es Salaam today.

East African artists for Nairobi Concert

Word in town is that there will be a mega concert in Nairobi on 6th December 2008, during which the curtain will be pulled off a fresh and new movement for the young folks which is causing a huge buzz in Nairobi. We have established that the movement known as Generation Jipange has attracted the interest of top performers from Uganda and Tanzania.

Generation Jipange, is the latest craze in town, a new culture for the youth, that youngsters are positioning themselves to be part of this phenomenon which promises to change their lives and will redefine the youths lifestyle as we know it today.

This one of a kind music concert will be held in Nairobi at Uhuru Gardens, Langata road. The concert kicks off at 9 am till 6pm and it is FREE FOR ALL. No gate charges.

Some of the local Kenyan artists who will be performing at the concert include Mejja, Jimwat, Maddtraxx, award winning Juacali, MTV Africa Music Awards winner Wahu, Wyre, Big Pin, and recent Channel O music awards nominees Nameless and Amani, M.O.G., Sarakasi and Sina X..

Tanzania will be represented by TMK Wanaume, THT Dance Group and Professor J, while the eccentric Bebe Cool will be in Nairobi to share the stage wtih Klear Kut also from Uganda.

We have confirmed that the top cream of Nairobi’s hottest DJ’s are not missing this one. They will be playing in the all day long music fest among them M.O.B., HomeBoyz, CodeRED, Black Supremacy and the Dohty Family

To keep the concert rocking and kicking all day long and to tell you more about the Jipange, MCs Big Tedd, Porgie, KJ, Kriss Darling and Eve D'Souza will take turns at the microphone to liven up the day as the coolest guys join Generation Jipange.

Tuesday, November 25, 2008

Mramba, Daniel Yona kizimbani kwa ufisadi







MAWAZIRI wawili waliowahi kuongoza wizara mbalimbali ikiwamo nyeti ya fedha katika serikali ya awamu tatu, Basil Mramba na Daniel Yona wamefikishwa kortini kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Mramba na Yona walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana mbele ya Hakimu Hezron Mwankenja saa 5.40, wakasomewa mashtaka na baadaye kupelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Vigogo hao walifikishwa mahakamani baada ya uvumi wa tukio hilo kudumu kwa takribani majuma mawili.

Wakati wakiingia mahakamani jana Mramba ambaye ni mtuhumiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 1200 ya mwaka huu, alisikika akiwahoji waandishi iwapo wamefurahi kufikishwa kwao mahakanai hapo, huku akidai kuwa watapiga picha

Sunday, November 23, 2008

Mambo ya ngorongoro





Kuna mambo makubwa huko Ngorongoro mdau Alphan Mlacha alikuwapo huko kwa takribani wiki nzima akiwa katika ziara ya kikazi iliyomwezesha yeye na wadau wengine wa habari ambapo walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi hiyo ya taifa ambayo ina umaarufu mkubwa duniani, juu kabisa waweza kuwaona wamasai wakiwa karibu kabisa na maboma yao, kisha picha zinazofuata zinaonyesha uoto wa wa asili na maboma mengine hii ziara mdau mlacha aliifanya juzi tuu.

Monday, November 17, 2008

msimu wa machungwa


Mfanyabiashara katika eneo la mnada wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro akipanga machungwa chini ya ardhi huku akipingana na utaratibu wa kutofanya biashara ya matunda katika mnada huo. machungwa hayo alikuwa akiuza kwa fungu sh 300. (Picha na Juma Ahmadi, MSJ).

mgomo wa walimu noma


PPichani wanafunzi wa shule ya msingi, Kiranyi na Unyuata wilayani Arumeru wakiwa wanacheza ovyo baada ya walimu wao kuanza mgomo jana.
picha na mussa juma


Wednesday, November 12, 2008

Uingereza yabana masharti ya viza

KWA wale wanaotaka kwenda Uingereza bila ya mipango ya muda mrefu, sasa wanatakiwa kujipanga upya; Uingereza imeongeza masharti mapya na magumu ya viza duniani kote.

Watanzania wanaokadiriwa kuwa kati ya 8,000 na 9,000 huomba visa ya kuingia taifa hilo kongwe kila mwaka, lakini masharti hayo mapya yanaweza kufanya idadi hiyo kupungua.

Moja ya masharti hayo ni lile linalomtaka Mtanzania yeyote anayetaka kuingia Uingereza, kama ilivyo kwa raia wengine wote wasio Waingereza duniani kote, sasa anapaswa kuwasilisha maombi ya viza wiki sita kabla ya siku ya safari.

"Ubalozi wa Uingereza hautakuwa tena na uwezo wa kuwezesha upatikanaji wa viza, ikiwa mwombaji atatoa taarifa ya muda mfupi," alisema afisa habari wa ubalozi wa Uingereza nchini, John Bradshaw.

Chuo Kikuu watimuliwa









UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi ya Mlimani umewasimamisha masomo wanafunzi wa shahada za kwanza kwa muda usiojulikana.

Hatua hiyo imekuja baada ya wanafunzi hao kukaidi amri ya chuo pamoja na ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof Jumanne Maghembe, iliyowataka kusitisha mgomo na kurudi madarasani wakati wizara ikishughulikia madai yao.

Kufuatia hatua hiyo, Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Anthony Machibya, aliwatangazia wanafunzi wenzake juu ya kusimamishwa huko na kusisitiza kuwa, pamoja na kufukuzwa chuoni hapo, lakini watakaporudi wataendeleza harakati za kudai haki yao mpaka watakapoipata.

Tuesday, November 11, 2008

Miriam Odemba akuna wengi Miss Earth


MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Earth, Miriam Odemba ameibuka mshindi wa nafasi ya pili katika kinyangíanyiro hicho kilichofanyika Jumapili usiku kwenye ukumbi wa Clark Expo Amphitheater, Angeles City, Pampanga nchini Philippines.

Hii ni mara ya kwanza tokea kuanzishwa kwa mashindano hayo kwa Mtanzania kumaliza katika nafasi ya juu na ni mara ya pili katika Afrika kushika nafasi hiyo ya juu kabisa katika mashindano hayo.

Nyota ya Odemba ilianza katika mashindano ya awali ambapo alifanikiwa kutwaa tuzo ya Miss Aficionado. Ameibuka mshindi wa kipengele cha masuala ya mazingira kinachohusu hali ya hewa.

Mrembo wa Kenya, Winfred Omwakwe alishinda taji la Miss Earth mwaka 2002 mjini Manila na kuweka historia kuwa msichana wa kwanza kutwaa taji hilo duniani.

ìNina furaha kubwa kutwaa nafasi hii, niliandaliwa kushinda na nimeshinda, namshukuru Mungu na pia mwandaaji wangu, Sarungi (Maria) kwa kunipa nafasi hii ya kuiwakilisha taifa na kufanikiwa kutwaa nafasi hii, nawashukuru Watanzania wote walionipa sapoti kubwa kabla ya mashindano,î alisema Odemba kwa njia ya simu jana baada ya kuisha kwa mashindano hayo.

Alisema kuwa ushindi huo ni sifa kwake, kwa Kampuni ya Compass Communication chini ya Maria Sarungi na Tanzania nzima kwani lengo lilikuwa kuipromoti Tanzania nje ya mipaka na lengo limetiamia.

Kwa mujibu wa Odemba, mashindano hayo yalikuwa magumu sana na alijitahidi na kutumia uwezo wake wa kimataifa kufanya vyema.

Katika mashindano hayo, mrembo wa Philippines Karla Henry, 22, alifanikiwa kutwaa taji hilo kwa kuwashinda warembo 84 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Miss Mexico, Abigail Elizalde alishinda nafasi ya tatu wakati ya nafasi ya nne ilichukuliwa na mrembo wa Brazil, Tatiane Alves.

Warembo nane bora wa mashindano hayo ni Mariana RodrÌguez (Colombia), Adriana ReverÛn (Hispania), Nasanin Nuri (Uswisi) na Daniela Torrealba wa Venezuela.

Warembo 16 bora wa mashindano hayo ni Hana Svobodov· (Jamhuri ya Czech), Seo Seol-hee (Korea), Uko Ezinne (Nigeria), Karolina Filipkowska (Poland), Ruxandra Popa (Romania), Anna Mezentseva (Russia), Piyaporn Deejing (Thailand), Jana Murrell (Marekani)

Habari hii ni kwa mujibu wa Majuto Omary wa The Citizen

R.I.P Miriam Makeba


A South African singer Miriam Makemba died 76.

She was an amazing icon.
A strong woman who took African music to the next level.

Not only South Africa, but the all Africa continent will always be proud of you.

May Lord rest her soul in peace. Amen!
(March 4, 1932-November 9,2008)

Monday, November 10, 2008

Msanii kutoka nchini Marekani Kat De Luna











Msanii kutoka nchini Marekani Kat De Luna usiku wa kuamkia leo alikonga nyoyo za wabongo katika tamasha kubwa la Fiesta 2008’ Jirambe’ baada ya kupiga shoo ya kufa mtu na kuwafanya wanazi wa burudani waliokuwa wamefurika katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam kumshangilia muda wote. Vibao vyake vya Am I Dream’ng na Run the Show ndivyo vilivyowadatisha wengi na kuwafanya mashabiki hao kuimba naye sambamba.

Sambamba na mwanadada huyo, pia kijana kutoka Dodoma ‘East Zuu’ Albert Mangwea ‘Ngweair’ akiwa sambamba na msela wake Mchizi Mox waliwakimbiza vilivyo mashabiki. Wasanii wengine waliokamua ni Ali Kiba, Mr.Blue, Profesa Jay, Nakaaya,Q Jay, Q Chief, Mwasiti, J-Moe, Bushoke, makundi ya TMK Wanaume Family na Halisi, bendi ya FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’ na wengine kibao waliofanya mashabiki kujiramba.

Thursday, November 06, 2008

Vurugu chuo kikuu




Unaona hapa ni kama vile kuna vita, wala si watu wengine bali ni wanafunzi wa Chuo KIkuu cha Dar es salaama wakipambana wao kwa wao ambapo wamewajeruhi wenzao kwa mawe na chupa katika harakati za kuwaondoa wengine madarasani.

Tukio hilo lilisababishwa na vurugu kati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliogoma wakitaka wapewe asilimia 100 ya mikopo inayojumlisha fedha za kujikimu na ada za masomo na baadhi yao ambao walipinga mgomo huo, baada ya waliogoma kuwalazimisha wenzao kutoka madarasani.

Wanafunzi wawili wamelazwa katika zahanati ya chuo ambao ni Makala Simon mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia ambaye amepigwa jiwe na kujeruhiwa shavu la kushoto.

Pia yupo Benedict Edward aliyejeruhiwa kichwani baada ya kupigwa chupa ya soda kichwani ambaye hali yake ilizidi kuwa mbaya na akapelekwa hospitali ya Misheni Mikocheni kwa matibabu zaidi.